Mganga afariki baada ya kunywa dawa iliyomuuwa mgonjwa wake






Zambia. Edith Chilanda (59) mwanamke aliyekuwa anaumwa mguu amefariki dunia baada ya kupewa dawa ya mitishamba na mganga aliyemwendea ili amponye.

Mganga huyo aliyefahamika kwa jina la Kapoya Chiyesu alimpa dawa za mimea mteja wake huyo aliyekuwa amevimba mguu ambapo baadaye alianza kutapika na kukimbizwa hospitalini ambapo alifariki kabla ya kupatiwa matibabu.

Baada ya sakata hilo wanakijiji na familia ya marehemu walimfuata mganga awaeleze kilichosababisha ndugu yao apoteze maisha.

Katika kuthibitisha kuwa dawa aliyompa marehemu haikuwa na sumu wala madhara yeyote na yeye akainywa mbele za watu hao, lakini bahati mbaya mganga na yeye akapoteza uhai kama marehemu Chilanda.

Kulingana na Ofisa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini-Magharibi, Dennis Moola, amesema Chiyesu alikunywa mchanganyiko huo naye akaanza kutapika akawaishwa katika hospitali ya Wilaya ya Kabompo lakini alifariki mara alipofika.

"Polisi walitembelea nyumba ya marehemu Chilanda na kukusanya mizizi yote pamoja na mimea iliyokatwa katwa kwenye sufuria ambayo inasadikiwa kuwa waliyotumia marehemu wote," amesema Moola.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad