Mwanariadha wa Kenya Faith Kipyegon aliweka rekodi mpya ya dunia ya mita 1500 katika mashindano ya Florence Diamond League siku ya Ijumaa.
Muingereza Laura Muir alikuwa mita 10 nyuma ya bingwa mtawala wa Kenya na bingwa wa Olimpiki, 29, kuelekea mkondo wa mwisho.
Naye Kipyegon alifuzu kwa ushindi katika dakika 3 sekunde 49.11, na kuvunja kizuizi cha 3:50 kwa mara ya kwanza, huku Muir akikimbia kwa muda bora wa msimu wa 3:57.09.
Genzebe Dibaba wa Ethiopia aliweka rekodi ya awali ya saa 3:50.07 mwaka 2015.
Ciara Mageean wa Ireland pia alikimbia wakati bora zaidi wa msimu alipomaliza wa nne kwa 4:00.95.
Kipyegon ameshinda dhahabu ya dunia na Olimpiki mara mbili lakini hii ni mara yake ya kwanza kuvunja rekodi ya dunia