Mkurugenzi TPA: Bunge Lisiporidhia, Mkataba na DP World Hautakuwepo



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa, amesema Bunge la Tanzania lina Haki ya kuridhia au kutoridhia Mkataba wa ushirikiano wa Kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari(IGA)

Amesema, "Kama Bunge halitaridhia Mkataba huu hautakuwepo kwasababu una sharti lazima uridhiwe. Bila kuridhia utatekeleza kwa nguvu ipi?. Maelekezo yoyote ya kurekebisha vifungu vya Mkataba huo kutoka #Bungeni, yatatafsiriwa ni kutoridhiwa kwa Mkataba

Mkataba huo ulisainiwa Oktoba 25, 2022 kati ya Serikali ya #Tanzania na Serikali ya #Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa Miundombinu ya kimkakati ya Bandari za Bahari na Maziwa Makuu, Maeneo Maalumu ya Kiuchumi, Maegesho ya Utunzaji Mizigo na Maeneo ya Kanda za Kibiashara

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad