Muuguzi Hospitalini Ambaka Binti Aliyekuwa Amelazwa Hospitalini


Muuguzi Hospitalini Ambaka Binti Aliyekuwa Amelazwa Hospitalini

Muuguzi mmoja wa Hospitali ya Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora anatuhumiwa kumbaka Binti mmoja (jina limehifadhiwa) Mgonjwa aliyekuwa amelazwa Hospitalini hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Simon Chacha amesema tukio hilo limetokea usiku wa June 9, 2023 katika Hospitali hiyo wakati Binti huyo alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Malaria na UTI.

Chacha amesema baada ya tukio hilo Serikali imechukua hatua za kinidhamu kwa kumsimamisha kazi Muuguzi huyo na kwamba Polisi wapo katika hatua za mwisho za uchunguzi kabla ya kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad