Mwanafunzi wa Sekondari Pandahill Adaiwa Kupotea Akikimbia Adhabu Shuleni




Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Mchepuo wa PCB, Shule ya Sekondari Pandahill hajulikani alipo baada ya kudaiwa kupotea zaidi ya mwezi mmoja uliopita wakati akikimbia adhabu kutoka shuleni hapo

Sauti inayodaiwa ni mzazi wa Mwanafunzi mtoto huyo inaeleza kuwa, maelezo hayo yametolewa na Shule husika licha ya kuwa kuna mazingira tatanishi. Pia, inadaiwa kuwa kabla ya kupotea Ester aliandika barua ambayo ndani yake aliandika “Naomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanya Wanafunzi kuwa na maisha magumu kama alivyonifanyia mimi.”

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Afisa Elimu Mbeya (Sekondari), Ernest Hinju amesema “Ni tukio la kweli, lipo chini ya Jeshi la Polisi, wanapeleleza na ndio wana majibu lakini bado Mtoto hajapatikana.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad