Mwanamke Aliyefariki Akutwa Akipumua Kwenye Jeneza Siku ya Mazishi yake


Waombolezaji katika mazishi ya mwanamke mzee wa Ecuador walishtuka kugundua kuwa bado yu hai.

Bella Montoya, 76, alitangazwa amefariki wiki iliyopita kufuatia kile kinachoshukiwa kuwa kiharusi.

Saa tano usiku wa kuamkia Ijumaa, jamaa wakijiandaa kubadilisha nguo zake kabla ya mazishi walimpata akihema.

Bi Montoya sasa amerejeshwa hospitalini akiwa katika uangalizi mahututi, na wizara ya afya ya Ecuador imeunda kamati kuchunguza tukio hilo.

Katika taarifa, wizara hiyo ilisema kwamba mwanamke huyo alipatwa na mshtuko wa moyo – awaka hawezi kupumua na matatizo ya moyo - na hakuonyesha dalili za kuamka wakati wa majaribio ya kumsaidia kupata tena fahamu.

Daktari wa zamu alithibitisha kifo chake.

Mwanawe, Gilber Rodolfo Balberán Montoya, alinukuliwa na vyombo vya habari vya ndani akisema kwamba mama yake "alilazwa mwendo wa 09:00 asubuhi na saa sita mchana daktari aliniambia [amefariki]".

Kisha Bi Montoya aliwekwa kwenye jeneza kwa saa kadhaa hadi alipoonekana na wanafamilia akijaribu kupumua.

Video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii ilimuonyesha akiwa amelala kwenye jeneza lililo wazi na akipumua kwa nguvu huku watu kadhaa wakiwa wamemzunguka.

Wahudumu wa afya kisha wanaonekana wakiwasili na kuanza kumfuatilia Bi Montoya kabla ya kumsogeza kwenye machela na kumuingiza kwenye gari la wagonjwa.

Sasa yuko katika uangalizi mahututi katika hospitali hiyo hiyo ambapo madaktari walitangaza kifo chake.

Shirika la habari la AFP lilimnukuu Bw Balberán akisema: "Kidogo kidogo ninaelewa kilichotokea. Sasa ninaombea tu afya ya mama yangu iendelee kuimarika. Namtaka awe hai na awe kando yangu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad