Kocha Nasreddine Nabi amefichua kwamba Bilionea wa Yanga, Ghalib Said Mohamed 'GSM' amempa
mwaliko rasmi kwamba atafurahi kumuona kwenye Tamasha la kilele cha Wiki ya Wananchi cha msimu huu.
Nabi alisema endapo atakuwa hana ratiba ngumu atarudi haraka kuja kuungana na familia yake kwa kuwa Yanga ni watu wake alioishi nao kwa furaha.
"Nilipokwenda kumuaga bwana Ghalib aliumia, nami niliumia sana, unajua Ghalib alinipa heshima kubwa sana wakati wote niko hapa nilikuwa sehemu ya familia yake kama ambavyo anaishi na ndugu zake," alisema Nabi na kuongeza;
"Hata hatua ya mafanikio ambayo tumeyapata huyu ndiye mtu aliyewezesha yote, amenialika nije kwenye kilele cha wiki ya wananchi nakuhakikishia kama sitakuwa na ratiba ngumu yoyote nitarudi hapa kuja kuungana na familia hii."