Nandy Hakumuandaa Yammi kabla ya Kumtambulisha, Adaiwa Hajui Kufanya Show na Kujibu Maswali ya Waandishi

 

Nandy Hakumuandaa Yammi kabla ya Kumtambulisha, Adaiwa Hajui Kufanya Show na Kujibu Maswali ya Waandishi

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO leo @el_mando_tz amezungumza kuhusu lebo pekee nchini inayomilikiwa na msanii wa kike na yenye lengo la kusaini wasanii wa kike pekee nchini inayomilikiwa na msanii The African princes Nandy.


@ei_mando_tz ametusanua kuwa Nandy alifanya haraka sana kufungua na lebo na kusainni msanii ambaye ni Yammi akiwa chini ya lebo yake ya The African Princes Label na akiwa ndio msanii pekee kwenye lebo hiyo.


@el_mando_tz anaeleza kuwa moja ya wasanii wa kike wenye kipaji cha hali ya juu cha kuimba na kuadika nyimbo ni Yammi aliyechini ya Nandy lakini kunna vitu ambavyo vinafanyika na kuonekana Nandy hakumuandaa Yammi au alikuwa na haraka sana kumsaini.


Anatolea mfano wa namna lebo zingine zinavyochukua muda mrefu kutambulisha wasanii wake mfano WCB ambayo inachukua hata miaka miwili kumpa darasa msanii wake kabla ya kumtambulisha kwenye jamii.


Lakini pia Vanillah wa Kings Music ambaye alichukua muda mrefu bila kutambulishwa na Alikiba mpaka ilifikia muda akawa anamuandikia mpaka boss wake nyimbo akiwa tu anafundishwa baadhi ya vitu.


Mara nyingi wasanii hawa wakitambulishwa huwa tayari wameiva katika kila idara, angalia mfano wa Zuchu na Vanillah, ni aina ya wasanii waliokamilika kwani walifundwa kabla ya kutambulishwa.


Tatizo linakuja kwa upande wa Nandy, kwa namna msanii wake anafanya na anavyoshirikiana na wasanii wenzake pia kwenye upande wa kufanya show, hasa show zake kadhaa alizofanya na hata kujibu maswali alipokuwa anafanyiwa mahojiano unagundua kabisa kuna vitu Yammi alitakiwa apewe darasa kwanza kabla ya kutambulishwa.


Hii inamaana kuwa Nandy alikuwa na haraka sana kufungua lebo na kumtambulishwa msanii kwa muda mfupi, na yote inawezekana nni kwa sababu alikuwa anashindanishwa na Zuchu hivyo alitafuta namna ya kujitofautisha na Zuchu, ambacho sio kitu kibaya.


@el_mando_tz anamaliza kwa kusema kuwa bado mapema sana Nandy ana nafasi ya kumuweke chini na kumfunza namna ya kuendana na soko la muziki linavyotaka hata kuingia kwenye ushindanni kwa baadhi ya wasanii.


Hayo ni maoni yake @el_mando_tz unakubaliana naye au hukubaliani naye?? ni kwanini??

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad