Polisi Wanane Wafariki Katika Mlipuko wa Gari



Takribani Maafisa wanane wa Polisi nchini Kenya, wameuawa wakati gari lao kushambuliwa na kilipuzi katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na Kundi la Waislam wenye itikadi kali wa Al-Shabab wanaoishi nchini Somalia.

Shambulizi hilo, lilitokea katika kaunti ya Garissa mashariki mwa Taifa hilo, eneo linalopakana na Somalia ambapo Al-Shabab wanaendesha uasi wa umwagaji damu dhidi ya serikali dhaifu ya Mogadishu kwa zaidi ya miaka 15.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki, John Otieno amesema “tumepoteza maafisa wanane wa polisi katika shambulio hili, tunashuku al Shabab ambao sasa wanalenga vikosi vya usalama na magari ya abiria.”


Jeshi la Kenya liliingilia kati mwaka wa 2011 nchini Somalia kupambana na al Shabab. Vikosi vyake vilijiunga mwaka 2012 na kikosi cha Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia (AMISOM, ambayo kwa sasa inaitwa ATMIS), ambacho kiliwatimua Al Shabab kutoka katika ngome zao kadhaa.


Tangu mwaka 2011, Kenya imekuwa mlengwa wa mashambulizi kadhaa mabaya yaliyodaiwa na Al Shabab, hasa dhidi ya kituo cha ubiashara cha Westgate huko Nairobi (Septemba 2013, watu 67 waliuawa), Chuo Kikuu cha Garissa (Aprili 2015, watu 148 waliuawa) na hoteli ya Dusit ( Januari 2019, watu 21 waliuawa).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad