Profesa Janabi atoa mbinu kupunguza kitambi




Dar es Salaam. Unapohitaji kuondoa kitambi ‘flat tummy’ unajua kwamba unatakiwa kula pale tu unaposikia njaa? Utamaduni wa walio wengi ni lazima ale asubuhi, mchana na usiku hali inayochangia uzito uliozidi, vitambi na magonjwa yasiyo ambukiza (NCD).

Wataalamu wamesisitiza watu wanatakiwa kula pale wanaposikia njaa na kutokuwa na milo midogo midogo ya mara kwa mara, huku wakitakiwa kula mlo wa jioni saa 12 ili kufanya uchakataji mapema kabla ya muda wa kulala.

Hayo yamesemwa jana Jumanne, Juni 20, 2023 na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi wakati akifungua mdahalo wa kujadili masuala ya kiafya ‘Health Awareness Talk’ ulioandaliwa na kampuni ya Medeviva ukiwashiriksha madaktari kutoka Tanzania na India.

Amesema chakula kingi, kisicho bora na bila kipimo ni chanzo cha vitambi, uzito kupita kiasi ambao huzaa magonjwa ya shinikizo la damu ambalo huzalisha magonjwa ya moyo, ini na baadaye magonjwa ya figo.

“Kitu cha kwanza ni nidhamu ya kula, umekula chakula cha mchana kwa sababu una njaa au unakula tu? Umewahi kujiuliza kwanini unakula na huna njaa? Hicho chakula kinaenda tumboni ambako kuna kingine bado kinachakatwa, haitakiwi na haishauriwi.

“Kwanini watu wanaingia katika kupunguza uzito ni kwa sababu wamekula sana, unaamka asubuhi unakula hujasikia bado njaa na unachokula hakina mpangilio wa lishe bora, hakuna matunda wala mbogamboga,” amesema Profesa Janabi ambaye pia ni mshauri na mtaalamu wa magonjwa ya moyo.
A
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad