Rais Ruto aitaka Afrika kutotumia Dola katika mikataba ya kibiashara



Rais wa Kenya, William Ruto ametoa ushauri huo kwa viongozi wa Afrika akisema ni muda wa kuanza kuchukua hatua ya kuachana na malipo ya fedha kwa kutumia Dola ya Marekani badala yake kuwepo na mfumo wa malipo wa Pan-African Payments System (PAPSS)


Amesema mfumo wa PAPSS uruhusu kufanyika malipo kwenda nje kwa kutumia fedha za ndani ya Nchi lakini thamani ya kile kinacholipiwa kinabadilika kulingana na thamani ya fedha ya sehemu husika badala ya wote kulazimika kutumia Dola


Ruto amesema “Tunapata tabu kufanya malipo ya huduma na bidhaa kwa kuwa kila nchi ina fedha zake, hatuna haja ya kuwa na Dola wala kuhamia kutumia fedha nyingine kama ya China, tukitumia PAPSS itasaidia biashara kufanyika kwa urahisi.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad