Kupitia kwenye kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumza namna ambavyo msanii wa muziki wa Bongo Fleva Rayvanny anavyoshuka kimuziki kila kukicha.
@el_mando_tz anatusanua kuwa ukianngalia Rayvanny wa miaka miwili nyuma sio Rayvannny huyu wa sasa ambaye ametoa EP ya Flowers III huku kukiwa kama hakuna kitu kilichotokea haliyakuwa Rayvanny alikuwa akitoa nngoma moja tu kila kona inasikika.
Mbali na hilo @el_manndo_tz amehoji ni kwanini ngoma nyingi za Rayvanny ambazo zinafanya vizuri zinakuwa ni collabo?? na kwanini ile Collabo na Diamond?? inawezekana wasanii wote waliopitia WCB Rayvanny ndio mwenye collabo nyingi zaidi na Diamond na collabo zote zimefanya vizuri.
Imekuwa ngumu sana siku hizi Rayvanny kufanya nyimbo ya pekee yake na kufanya vizuri kama ilivyokuwa zamani.
@el_mando_tz anahoji kuwa inawezekana ni upepo wa kutoka WCB umemuathiri?? au inawezekana Rayvanny amerizika?? kwa sababu kila ukimtazama Rayvanny humuoni akikuwa kimuziki na kurudi kama Rayvanny wa miaka miwili mitatu nyuma.
Ameongeza kuwa katika nafasi ambayo Rayvanny aliipata na asingetakiwa kuichezea ni kufanya collabbo na Maluma ilikuwa ndio tobo lake Kimataifa.
Wewe unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??