Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kupitia, kuchambua na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto za Wafanyabiashara nchini.
Taarifa hiyo imekabidhiwa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema, Kamati hiyo imefanya kazi kubwa na imeleta majibu ambayo yatatatua changamoto za wafanyabiashara nchini.
Ameahidi kuwa Serikali imepokea taarifa hiyo na itayafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na kamati hiyo.
Kamati hiyo kwa ajili ya kupitia, kuchambua na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto za Wafanyabiashara nchini ambayo ilipewa siku 14, imefanya mapitio katika maeneo mbalimbali ya kikodi, bandari na maeneo ya wafanyabiashara kwenye mikoa