Sababu ya Jonas Mkude Kutemwa Simba yatajwa, Simba Wausingizi Muda

Sababu ya Jonas Mkude Kutemwa Simba yatajwa, Simba Wausingizi Muda


SIMBA SC ikiendeleza kutoa 'Thank You' kwa wachezaji wake kikosini , leo imetoa tamko kuhusu kiungo Jonas Mkude aliyedumu miaka 13.


Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika kuwa muda ndiyo umetenganisha mapenzi ya timu hiyo na Mkude.


"Ameondoka mtu tunayempenda kweli, ameondoka mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu. Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda,"


Ahmed katika andiko hilo amedai wakati Simba ina njaa, Azam ilimuhitaji Mkude ila hakuenda, Yanga walimtaka hakuenda akachagua kuvumilia njaa na kumpongeza kuwa ni zaidi ya mchezaji.


"Sisi tulitamani Mkude amalizie mpira wake Simba kwani hatutaki kucheza nae akiwa timu nyingine,  kwa sababu tukimfunga ataumia na yeye akitufunga ataumia hatuko tayari kumuumiza Mkude wetu," ameeleza Mkude akiongeza;


"Tumetoa taarifa ya kuachana nae punde tutatoa taarifa ya kumuaga na tutamuaga kwa heshima zote

, sisi ndo tunatambua zaidi heshima ya Mkude kuliko mtu mwingine yeyote na tutamuaga kwa heshima hiyohiyo,"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad