Sehemu ambayo vitunguu ni ghali zaidi kuliko nyama





Katika maeneo mengi duniani vitunguu ni chakula kikuu huku nyama ikisemekana kuwa anasa zaidi, lakini nchini Ufilipino bei ya vitunguu imepanda sana kuliko ile ya kuku na nyama ya ng’ombe.

Tabia ya kukaanga na vitunguu saumu na vitunguu maji katika nchi ya Asia ilianza wakati wa ukoloni wa Uhispania, ambao ulidumu kati ya 1521 na 1898 na kuathiri sana mapishi ya vyakula vya nchi ya Asia

bidhaa ya anasa kwa Wafilipino ni vitunguu  na hii. Ni Baada ya kupanda kwa bei, bidhaa hiyo inagharimu zaidi ya nyama aina nyingi tu.

Kilo moja ya vitunguu vyekundu na vyeupe ilifikia takriban $11 zaidi ya sh elfu 25 huku kuku mzima angeweza kununuliwa kwa karibu $4 yaani elfu Tisa hivi


Katika eneo moja huko ufilipino linaloitwa cebu Bei ya vitunguu zilishuka kidogo, kwani  vitunguu vyekundu na vyeupe vilikuwa vikiuzwa kwa bei ya ($10.88)  yaani tsh 25,698 kwa kilo

Hiyo bado ni zaidi ya mara mbili ya bei ya kuku na 25% na 50% ya bei ghali zaidi kuliko nyama ya ng’ombe, kulingana na data rasmi ya ufuatiliaji wa soko.

Ufilipino ni nchi inayoagiza vitunguu kutoka nje – hutumiwa zaidi kuliko inavyozalishwa Pamoja na vitunguu saumu, vitunguu maji ni viungo muhimu kwa vyakula vya Ufilipino.


Utamaduni huu umesababisha Vyakula vingi mitaani huko Cebu kuweka vitunguu katika milo mingi ya nchini Ufilipino

Kwaheri Chokoleti, karibuni vitunguu swaumu.  [vitunguu] vina uwezo wa kuwa zawadi nzuri ya kuleta nyumbani nchini Ufilipino,” Mfilipino mmoja anayeishi Marekani alichapisha ujumbe huo kwenye Twitter.


“Tunaleta vitunguu badala ya chokoleti kutoka kwenye safari yetu

 Vitunguu vinajulikana kuwa na vioksidishaji  ambayo husaidia kupambana na kuvimba, kuzuia triglycerides, na kupunguza viwango vya cholesterol – yote haya yanaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Sifa zao zenye nguvu za kuzuia uchochezi zinaweza pia kusaidia kupunguza shinikizo la damu na kulinda dhidi ya kuganda kwa damu.

Aina nyingi za vitunguu vina kemikali zinazojulikana kusaidia kupambana na saratani, pia.

Vitunguu ni miongoni mwa vyanzo vya chakula tajiri zaidi vya kirutubisho kinachoitwa quercetin, kinachojulikana kukataza shughuli au uundaji wa vitu vinavyosababisha saratani, kulingana na WebMD.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad