Serikali 'Leteni Taarifa za Madeni ya Waalimu"


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayesimamia elimu, Dkt. Charles Msonde ameagiza ndani ya siku saba Maafisa Elimu wa Wilaya nchini wabainishe madeni yote ya Walimu ikiwemo madeni ya likizo na uhamisho
na kuyawasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Dkt. Msonde ameeleza hayo leo tarehe 04 June 2023 wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Wilaya na Mikoa yote nchini cha kujadili na kutathmini utekelezaji wa vigezo vya upimaji wa elimu nchini (KPI) kilichofanyika Mkoani Tabora.

“Maafisa Elimu na Wakuu wa Idara wa Halmashauri tunawapa wiki moja mtuletee taarifa ya madeni yote ya Walimu ikiwa ni pamoja na ya likizo na uhamisho kwa kuyapanga kwa mwaka, na kila fedha inayoletwa kwa mwezi katika Halmashauri ya kulipa hayo madeni nijulishwe Waalimu wangapi wamelipwa na madeni yamebakia kiasi gani”

Msonde amesema Serikali imekuwa ikitenga na kutoa fedha za likizo na Uhamisho kila mara lakini fedha hiyo imekuwa haitolewi kwa haki ambapo yamekuwa yakilipwa madeni ya hivi karibu na madeni ya kipindi cha nyuma yanaachwa.

“Madeni haya tukiyalipa kwa haki, Walimu watapata faraja na kujua kuwa Serikali yao inawajali na imelipa madeni kiasi flani kwa mwaka husika na mwaka unaofuata Serikali itaendelea kupunguza madeni hayo kwa Walimu wetu”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad