Serikali ya Marekani Yakataza Raia Wake Kwenda Uganda Kisa Ushoga


Serikali ya Marekani imewaonya raia wake dhidi ya kusafiri kwenda Uganda kufuatia Uganda kupitisha sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja hivi majuzi.

Hatua hiyo inajiri wiki mbili baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuridhia sheria hiyo yenye utata licha ya onyo kutoka kwa viongozi wa dunia na wanaharakati wa haki za binadamu.

Katika taarifa iliyotolewa na idara ya mashauri ya nje na kuwekwa kwenye tovuti ya Ubalozi wa Uganda, serikali ya Marekani ilisema kuwa sheria hiyo ni tishio kwa wasafiri wa LGBTQI .

Ilionya kwamba wasafiri wanaweza kukabiliwa na mashtaka, kifungo cha maisha au hukumu ya kifo.

Ilani hiyo ya ngazi ya tatu ya usafiri inawataka wasafiri kufikiria upya kuhusu kwenda Uganda na kwamba wanaweza kuwa waathiriwa wa mashambulizi ya makundi hatari .

Wale wanaounga mkono haki na maisha ya LGBTQI + wanaweza pia kufunguliwa mashtaka na kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu.

Sheria ya Uganda ya kupinga mapenzi ya jinsia moja ya mwaka 2023 imelaaniwa na kuzingatiwa kuwa moja ya sheria kali zaidi za kupinga mapenzi ya jinsia moja duniani.

Sheria hiyo inatoa faini na na kifungo cha kuanzia miaka 14 hadi kifungo cha maisha hadi adhabu ya kifo kwa kesi zinazozingatiwa kuendeleza mapenzi ya jinsia moja .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad