Waliofungua kesi hiyo ni Mawakili Emmanuel K. Changula, Alphonce Lusako, Raphael J. Ngonde na Frank J. Nyalusi wanaituhumu Serikali kupitisha mkataba huo kwa maelezo kuwa hauzingatii maslahi ya Nchi
Waziri wa Ujenzi na Katibu Mkuu wanashtakiwa kwa kusaini Makubaliano na kuyapeleka Bungeni bila kushirikisha Umma kutoa maoni ikiwa ni kinyume na Kifungu cha 11(1)(2) cha Sheria ya Rasilimali za Taifa No. 5 ya mwaka 2017
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu wa Bunge wanashtakiwa kwa Kuliongoza Vibaya Bunge, Kupiga Kura ya Ndio ya Jumla badala ya Mbunge Mmoja Mmoja ambapo Washtakiwa wote wanatakiwa kufika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Julai 3, 2023