Shule ya Pandahill yatoa Tamko Sakara la Ester

 

Shule ya Pandahill yatoa Tamko Sakara la Ester

Uongozi wa Shule ya Sekondari Pandahill pamoja na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga ambaye ndiye mmiliki wa Shule unatoa shukrani za dhati na pongezi nyingi kwa: -

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake kuwezesha kupatikana kwa Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu.

Vyombo vya ulinzi na usalama na hasa kamati za ulinzi na usalama za Wilaya na Mkoa wa Mbeya, chini ya Mheshimiwa Komrade Juma Zuberi Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kwa kuwa bega kwa bega na Shule katika kipindi chote cha utafutaji.

Wananchi, kwa kuonyesha ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwezesha kupatikana kwake.

Aidha, uongozi wa shule hiyo pia umetoa rai kwa Wazazi/walezi wote kuwalea na kuwaongoza watoto kwa kufuata misingi ya Sheria, Dini,

Maadili, Nidhamu na Haki ili waweze kupambana na changamoto za maisha popote wanapokuwa. Lakini pia tunawasihi wanafunzi kuendelea kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Shule ili kurahisisha usimamiaji na ufuatiliaji wa nidhamu shuleni.

Jamii iendelee kuviamini vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na kutoa ushirikiano wa taarifa zaidi kuhusiana na tukio husika ili uchunguzi uweze kufanyika kwa haraka, uhuru na haki na endapo itabainika mtu/ watu kuhusika na tukio hili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad