Simba Kung'oa Winga Mganda Kutoka Vipers




HAKUNA namna. Mabosi wa Simba imewabidi kugonga hodi kwa mara nyingine tena kwa mabingwa wa Ligi Kuu Uganda, Vipers ili kuona kama wanaweza kupata huduma ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Milton Karisa, 27, ambaye ni pendekezo la kocha Roberto Oliveira 'Robertinho'.

Karisa aliyepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' iliyotoka kupsuka baoa 1-0 katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na mechi ya kufuzu fainali za Afcon 2023 dhidi ya Algeria itakayopigwa wikiendi hii, bado anna mkataba wa mwaka mmohja na klabu yake ya sasa.

Hata hivyo, imeelezwa mabosi wa Simba wametua maombi ya kuulizia namna ya kumsajili mchezaji huyo ili aitumikie timu hiyo kwa msimu ujao, huku wababe wa Rwanda, APR nao wakiingia mkono wakihitaji pia huduma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Uganda, inaelezwa kuwa Simba imeonyesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo ambaye alikuwa sehemu ya mafanikio ya Robertinho wakati akiinoa timu hiyo, ambapo chanzo kutoka Uganda kimethibitisha Vipers kupokea barua ya Simba ikiomba kumsajili Karisa.


"Hakuna kinachoshindikana, muhimu ni kukubaliana tu kwenye mazungumzo, tungependa kuendelea kuwa naye kwenye kikosi chetu lakini mchezaji mwenyewe naye ameomba kuondoka," kilisema chanzo hicho ambacho ni mmoja wa vigogo wa Vipers iliyokuwa kundi moja na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kupasuka nje ndani kwa bao 1-0 na kuonmgeza;

"Tumekuwa na vikao kwa ajili ya kujadili hiki ambacho kinaendelea nadhani wiki chache zijazo tutakuwa na maamuzi ya pamoja."

Taarifa nyingine kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa, kocha Robertinho ambaye kwa sasa yupo kwao Brazili kwa mapumziko mafupi, amekuwa akifanya mawasiliano ya siri na Karisa na kumweleza mipango aliyonayo juu yake kutokana na ukaribu baina yao.

Karisa yupo tayari kutua Simba, ikielezwa amepewa ofa ya kusaini mkataba wa miaka miwili ili kuungana na Robertinho aliyeiwezesha Vipers kutinga makundi ya michuano hiyo kabla ya kutua Msimbazi na kuiofikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa iking'olewa na waliokuwa watetezi Wydad Casablanca ya Morocco iliyoenda kupoteza taji kwa Al Ahly ya Misri wikiendi iliyopita.

Mwanaspoti lilimtafuta Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, lakini simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa, japo hivi karibuni alikaririwa kwamba klabu yao inaendelea kujipanga na kusajili kila mchezaji inayemhitaji kulingana na maelekezo ya kocha wao.

Mapema wiki hii klabu hiyo ilimsainisha mkataba wa miaka miwili, Winga Mcameroon, Leandre Onana ambaye mara aliposaini alitimka zake kwao ili kusubiri kuanza kwa kambi ya timu hiyo kujiandaa na msimu mpya wa sambamba na kushiriki Tamasha la Simba Day litakalomtambulisha.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad