Simba na Yanga, Dunia ya Viongozi na Mpango Kazi



Nini sababu ya anguko la Simba? Mashabiki wengi watakujibu kwamba Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya.

Ukienda kuwauliza Mashabiki wa Yanga, mna hofu gani? Watakwambia Coach Nabi, Fiston Mayele na Djigui Diarra wakiondoka wote ni issue haitokuwa rahisi, wengi watakujibu hivyo.

Kwenye Sports Xtra ya @cloudsfmtz nilikuwa na mtazamo tofauti! Kwangu Mimi kitu cha kutisha zaidi ni timu kupoteza Watendaji wake ama Viongozi, hicho ndio kitu hatari zaidi, mpira unachezwa zaidi ofisini kuliko uwanjani.

Kabla ya kuwa na hofu ya Chama, Bwalya ama Miquisson kuondoka lazima ujiulize swali waliletwa na nani? Je wapo? Kama hawapo nani wamerithi? Na wamerithi kwa plan ipi? Proper succesion plan in question.

Kabla ya kuwa na hofu ya Nabi kuondoka ama Fiston, maswali ni mepesi! Je nani alimleta Nabi, nani alimleta Mayele? Nani walikuwa wanawalipa? Kama wapo then succession itapatikana kwa njia zile zile walizotumia.

Niwape concept kidogo kuhusu Brighton apambo CEO Paul Barber alipoulizwa ipi siri nyuma ya Seagulls? Akawaambia tazama yale mafaili 20, ile ndio Brighton nzima! Hakutaja Wachezaji bali mipango ya Viongozi kwenye makaratasi.

Brighton wana mbinu zao kama Plan B, Wrinkles in Timing na Next Man Up kama mfano tu, waliwezaje kufanya biashara ya Leandro Trossard kwenda Arsenal kisha Kaioru Mitoma akavaa viatu? Ameondoka Cucu akaja Estupinan? Akaondoka Kocha Graham Potter akaja Roberto Di Zerbi aliewahi kutisha Sassoulo kabla ya Donetsk? Ni mpango kazi wa CEO.

CEO huyu alisema klabu haiwezi kuogopa kufanikiwa na haiwezi kuogopa kufanya biashara kwakuwa mpira ni mchezo wa ndoto na pesa, wamewekeza sana kwenye basics kuliko juu na wanavuna pesa nyingi sana.

Mashabiki wa Simba na Yanga, timu zenu hizi hazina nguvu kama Brighton dhidi ya Wababe ni lazima zitauza sana ila zinahitaji Viongozi imara sana, hivyo kama Viongozi wapo imara timu zitazidi kuwa imara!

Wachezaji huja na kuondoka, Makocha huja na kuondoka ila watasalia Viongozi na Mashabiki! Again kwakuwa Viongozi wapo wanapaswa kuwa na plans, STRONG LEADERSHIP.

By Farhan

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad