Simba na Yanga mpira umezidi kukuwa na Wachezaji wamezidi kuwa na majina makubwa kuanzia mitandaoni mpaka uwanjani, nafikiri ni wakati sahihi wa kuongeza zaidi mvuto kibiashara kwa kuchapisha jezi za Mashabiki zenye majina ya wachezaji sambamba na Wadhamini wake wote maana Mahaba yanazidi kukua.
Kuliko Shabiki pia kuishi kwenye ndoto ya kumiliki jezi ya Mchezaji fulani kwanini tusichukue hatua? Kuliko sometimes kuzifua jezi na kuzirejesha basi tuchukue jezi za mechi kadhaa ziuzwe kupitia Simba App ama Yanga App, issue ni watu kupreorder na klabu kuziweka jezi kwa mauzo zilizovaliwa ila kuzidi kuwasogeza Mashabiki kwa timu yao.
Mfano jezi aliyonipa Mchezaji bora wa muda wote Maestro Chama, nilipokea meseji nyingi watu wakiitaka jezi hadi kwa LAKI MBILI, nawaza klabu itaingiza kiasi gani wakizeweka hizo jezi zilizosainiwa mtandaoni na kuziuza, nawaza tu.
Klabu zetu ziitazame sana hii biashara ya jezi, imekuwa serious sana kwenye dunia ya mpira.
By Farhan