Simba Under 20 Aibu Kubwa...Yamaliza Ligi Bila Goli, Yashika Mkia


Simba ilishafanya uwekezaji kwenye soka la vijana na ikawalipa, walizalisha wachezaji wengi ambao walipata nafasi kwenye timu kubwa na ambao walishindwa kuingia kwenye timu ya wakubwa walienda timu nyingine wakacheza Ligi Kuu!

Bahati mbaya ile ilikuwa project ya watu wachache ndani ya klabu, haikubebwa na kutazamwa kwa picha kubwa na klabu.

Watu wenye maono waliibeba halafu Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akawa anawezesha kwa fedha kutoka mfukoni kwake.

Pata picha project ile ingeendelea hadi leo, Simba ingekuwa wapi? Wachezaji wangapi wangezalishwa? Simba ingepunguza gharama za usajili wa wachezaji wa ndani.

Lakini leo hii Simba U20 inamaliza ikiwa nafasi ya mwisho kwenye kundi lake [Kundi D] kwenye Ligi ya vijana [U20] tena ikiwa haijashinda mechi hata moja wala kufunga goli!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad