Licha ya kuoneshwa mlango wa kutokea katika Kikosi cha Simba SC, aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Nelson Okwa amelalamika kutolipwa stahiki zake mara baada ya kuvunjiwa Mkataba na Klabu ya Simba.
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu apewe “Thank You” Okwa ambaye ni raia wa Nigeria anasema;
“Mkataba wangu na Simba ulivunjwa kabla sijaenda Ihefu kwa Mkopo, jina langu liliondolewa hadi TFF kwenye orodha ya wachezaji wao, niliambiwa niende waone maendeleo yangu, lakini waliendelea kunilipa sehemu yangu ya Mshahara na Ihefu nao walikuwa wananilipa nusu.
“Naenda Nyumbani lakini bado nawadai, hata kuagwa mtandaoni (Thank you) Nilishangaa kwa sababu mimi sikuwa mchezaji wao. Nilienda Ihefu kufanya mazoezi tu kulinda kipaji changu lakini sio kucheza kwa ushindani.
“Mimi nimeondoka Nigeria nikiwa nahodha, nimecheza mchezo 1 tu wa Simba day, mechi zingine chache nilipewa dakikani 5, 4. Watu wameaminishwa sina uwezo kitu ambacho sio kweli. Simba wamekariri kikosi, Wachezaji ni walewale kila mara, hawafanyi rotation kama Yanga,” amesema Nelson Okwa
“Sisi tumeshamalizana na huyo mchezaji, tumemlipa pesa zake zote. Tumemuacha kwa kuwa hana uwezo. Simba wamepita makocha (3) yeye akiwa kikosini, lakini makocha wote walimuweka benchi kama angekuwa na uwezo basi hata kocha mmoja angempanga,” amesema Ahmed Ally, Meneja wa habari wa Simba SC