Issue ya Saudi watu wanaifananisha na China! Kuna misconcept sehemu kwanza sababu ya anguko la China kwenye project yao ni aina ya majina waliochukua haikuwa na mvuto huo! Oscar, Ramires, Hulk, Fellain, Dembele hawakuwa na profile kama Ronaldo, Kante, Benzema na wengine wengi.
Pili, China klabu zilikuwa na Matajiri wake ambao wengi ni Mabilionea baadae walianguka sana kiuchumi na kusimamisha uwekezaji mfano Jiangsu Suning walibeba CSL lakini afterwards walianguka, Mabilionea wa China hadi pale Inter Milan Bwana Steve Zhang akaanza kuanguka na kuuza wachezaji, uchumi uliyumba.
Unlike Saudi, juzi kati klabu nne Al Ahli, AlNassr, Al Ittihad na Al Hilal zimetangazwa kumilikiwa na Saudi Arabia's Public Investment Fund ambapo wana 75% huku 25% ikibaki kwa Wanachama as non profit, wao wamelenga uwekezaji, nguvu na biashara zaidi! Hii haikuwa sawa na China, hawa wamepita njia tofauti.
Saudia pia wakati huu wameboresha zaidi issue za Makocha wao wamepeleka sana Ulaya wakasome, wameboresha mifumo ya academies wakati huu wanafuatiliwa zaidi, ikumbukwe Waarabu mpira ni kipaji pia tofauti na China, Waarabu wana mahaba nao sana tofauti na China.
Ndio maana Ronaldo akasema kama wataendelea hivi kwa miaka mitano ijayo, hata Rais wa UEFA ameanza kuchukizwa na Saudia.