Tuzo za Grammy Zaitambua Bongo Flava Rasmi, Yaijumuisha Katika Mchakato

Tuzo za Grammy Zaitambua Bongo Flava Rasmi, Yaijumuisha Katika Mchakato


Tuzo za Grammy au maarufu kama Grammys, zinazotolewa na Recording Academy ya Marekani, wameongeza vipengele vipya vitatu kwenye Tuzo hizo kuanzia mwaka 2024.

Vipengele hivyo ni pamoja na Best African Music Performance, Best Alternative Jazz Album na Best Pop Dance Recording.

Ongezeko la ''Best African Music Perfomance'' ni habari njema kwa wasanii wa Kiafrika, hasa kwa muziki wa Afrobeats ambao umekuwa ukiliinua bara la Afrika kwa ujumla. Kipengele hicho kipya kimejumuisha Bongo Flava, Amapiano, Afro Beats na Aina zingine za music kutoka Afrika

Huwenda mwakani tukashuhudia wasanii wa Bongo Fleva wakichuana vikali na wasanii wengine kutoka Afrika katika kipengele hicho.

Awali, wasanii wa Afrika walikuwa wakigombea katika kipengele cha "Best Global Music Performance" katika tuzo za Grammy ambacho pia kitaendelea kuwepo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad