Unaambiwa Vumbi la Kongo Lapigwa Marufuku Tanzania

Vumbi la Kongo


Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limepiga marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa Dawa inayodaiwa kuongeza nguvu za kiume maarufu 'Akayabangu' pamoja na vumbi la Kongo kwa kile kilichoelezwa kuwa hazijathibitishwa ubora wake.


Kupitia taarifa yake kwa umma jana jumaa, Juni 23, 2023, Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Profesa Hamis Malebo amesema Baraza lilipata taarifa ya uwepo wa dawa hiyo ya Akayabagu ambayo haijawahi kusajiliwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, hivyo liliamua kufanya uchunguzi na kubaini dawa hiyo ina mchanganyiko wa dawa za kisasa kama Sildenafil (Viagra majina mengine Erecto ama Vega) jambo ambalo ni kinyume cha Sheria.


Aidha Baraza limepiga marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa VUMBI LA KONGO kote nchini na kuongeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka agizo hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad