Upepo Mkali, Mawimbi Makubwa Kuyakumba Maeneo Haya Kesho



Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetangaza utabiri ya kuwepo kwa hali mbaya ya hewa kuanzia kesho Jumatatu Juni 26, 2023 katika maeneo ya ukanda wa pwani wa bahari.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Juni 25, 2023 na mamlaka hiyo imeonyesha kutakuwa na upepo mkali na mawimbi makubwa katika pwani ya bahari ya Hindi.

“Angalizo la upepo mkali unaofikia km 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi,”imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imetaja maeneo ambayo yataathirika na hali hiyo ya hewa ni pamoja na; Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kupitia taarifa ya TMA iliyotolewa mchana wa leo Jumapili Juni, 25 imesema uwezekano wa kutokea ni wastani pamoja na kiwango cha athari zinazoweza kutokea pia ni wastani.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafirishaji baharini. Tafadhali zingatia na jiandae,” imetahadharisha taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad