Waliouawa shambulio la kigaidi Uganda wafikia 41



Uganda. Jeshi la Uganda limesema limeanza kuwasaka waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) wanaodaiwa kutekeleza mauaji ya watu 41 mpaka sasa huko Magharibi mwa nchi hiyo huku wengi wakiwa wanafunzi wa shule ya Sekondari.

ADF walivamia na kuuwa wanafunzi katika shule ya Sekondari Lhubiriha iliyopo Mpondwe mpakani na nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kutajwa kuwa ni mauaji mabaya zaid kuwahi kutokea katika kipindi cha muongo mmoja, maofisa wajeshi wamesema hayo jana Jumamosi Juni 17, 2023.

Jeshi limesema mbali na mauaji hayo pia ADF waliwateka nyara watu sita wakati wa uvamizi wa shule hiyo kabla ya kutoroka kurudi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Maofisa na mashuhuda walisema bunduki na visu vilitumika katika shambulio la usiku wa manane na mabweni ya wanafunzi kuchomwa moto katika shule hiyo iliyopo mji wa Mpondwe.


Akielezea mauaji hayo Meya wa Halmashauri ya mji wa Mpondwe-Lhubiriha, Sylvester Mapozi, amesema shambulio hilo liliwaua wanafunzi 39 na wakati washambuliaji wanarudi nyuma pia waliwaua watu wawili mwanamke na mwanamume. Hii inafanya idadi hiyo kufikia 41.

“Wengi wa waliofariki walichomwa moto kiasi cha kutotambulika huku wanafunzi wengine wakiwa bado hawajulikani walipo,”amesema Mapozi.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani vikali shambulio hilo, na kutuma rambi rambi zake kwa familia za waliopoteza wapendwa wao.


"Waliohusika na kitendo hiki cha kutisha lazima wafikishwe mahakamani," Msemaji wa Guterres amesema katika taarifa yake.

Ufaransa pia imelaani shambulio hilo katika taarifa ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje mjini Paris jana Jumamosi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad