Kijana Kepteni Warioba (23) amejiua kwa kujikata na mashine ya kupasua mbao leo Juni 16, 2023, Moshi mkoani Kilimanjaro, huku akiacha ujumbe wa kumtaka bosi wake aende kumzika mkoani Mara na asipofanya hivyo atakuwa akimsumbua mara kwa mara.
Tukio hilo limetokea leo Juni 16, 2023, katika mtaa wa Kalkacha, ambapo mashuhuda wamesema kuwa marehemu alikuwa mfanyakazi wa karakana ya kupasua mbao ya tajiri anayefahamika kwa jina la Erasto, ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Aidha mashuhuda wameongeza kuwa siku moja kabla ya tukio kulitokea kutoelewana baina yake na bosi wake baada ya kuonekana upotevu wa kiasi cha fedha ambacho hakijajulikana
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Kalkacha, Rau SweetFid Malewo amesema marehemu aliacha ujumbe kuwa mmiliki wakarakana hiyo akauzike mwili wake kwao mkoani Mara na asipofanya hivyo atakuwa akimsumbua mara kwa mara.