Watu 80 Raia wa Uganda Walioshawishiwa Kufunga Hadi Kufa Warudishwa Makwao




Simon Opolot, Mhubiri wa Kanisa la Wanafunzi wa Yesu, Uganda anatafutwa na Polisi baada ya kuwashawishi Waumini wake 80 kuwa Mwisho wa Dunia ulikuwa karibu hivyo kwenda Ethiopia, na kufunga kwa siku 40, ambapo wangemuona Yesu siku ya 41

Imeelezwa Waumini hao ambao wengi ni Walimu na Watumishi wa Umma waliacha Mali zao zote mapema 2023 na kisha kusafiri kutoka eneo la vijijini Mashariki mwa Uganda kwenda Ethiopia Kusini, umbali wa takriban kilomita 500 (maili 320)

Lakini mara tu Mamlaka za Ethiopia zilipojua kuhusu kuwasili kwao Machi 2023, walichukuliwa na kuhudumiwa na hatimaye kurudishwa Nyumbani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad