Watu Wanne wa Familia Wafariki Katika Ajali ya Boda Boda





Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia katika ajali ya barabarani kwenye barabara ya Malaba-Eldoret wakitokea mazishini Bungoma.


Katika taarifa iliyotolewa na Gavana wa Kakamega, Fernandes Barasa, Jumapili, Juni 4, ilibainisha kwamba familia hiyo ilikuwa ikisafiri kwenye pikipiki moja wakati walipokumbana na mauti yao.

Barasa alieleza kwamba lori lililokuwa limebeba mizigo liliteleza kutoka kwa barabara yake na kugongangana na pikipiki, na kuwaua wanne hao papo hapo.


Aidha, Gavana wa Kakamega alibainisha kuwa kati ya wanne hao, wawili walikuwa wanawake na wengine wawili walikuwa wanaume.


"Nimetarifiwa kwa huzuni kubwa kuhusu vifo vya kutisha vya wakazi wanne wa Kaunti ya Kakamega ambao walifariki katika ajali ya barabarani katika soko la Mayanja kwenye barabara ya Malaba-Eldoret wakati wakirejea nyumbani baada ya mazishi ya mpendwa wao katika Kaunti ya Bungoma.


"Waliofariki walikuwa wakisafiri kwenye pikipiki moja wakati lori lililokuwa limebeba mizigo lilipopinduka kutoka njia yake na kuwaua papo hapo," ilisoma sehemu ya taarifa hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wakazi wa soko la Manyanja waliiomba serikali kuweka vizuizi barabarani, wakisema kuwa wamekuwa wakishuhudia ajali nyingi kutokana na magari yanayopita kwa kasi.

Waliongeza kuwa walishatoa malalamishi yao kwa mamlaka husika, lakini bado mamlaka hizo hazikuchukua hatua yoyote.

"Kwa niaba yangu na wakazi wa Kakamega, ningependa kutoa pole zetu za dhati kwa familia zilizopatwa na msiba huu usioweza kurekebishwa na kuwaombea Mungu awape nguvu ya kustahimili hasara isiyoweza kufidiwa," aliongeza Barasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad