Yanga yawasili Algeria, wabeba vyakula na wapishi wao kukwepa hujuma



 Ili kuhakikisha wanakwepa hujuma za aina yoyote kutoka kwa wenyeji wao, Yanga imesafiri Algeria ikiwa kamili

Wananchi wameondoka na viroba vya vyakula, maji na wapishi wao ambao huwatumia wakiwa kambini Avic Town


Yanga ilijipanga mapema kwani baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya USM Alger uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais Arafat Haji na Mratibu Hafidh Saleh walitangulia Algeria

Imekuwa rahisi kwa Yanga ilipowasili Algeria haikukumbana na changamoto zozote kutokana na maandalizi yaliyofanyika kabla

Hii ni mechi muhimu kwa Yanga na Tanzania kwa ujumla, Wananchi wamejipanga kwa kila namna ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi siku ya Jumamosi na kutwaa taji la CAF CC
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad