Zari Hassan Awatolea Uvivu Wanaomsema Kisa Mumewe Shakib

 

Zari Hassan Awatolea Uvivu Wanaomsema Kisa Mumewe Shakib

Mwanasosholaiti na mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady' amewatolea uvivu wanaomsema mitandaoni kuwa ameolewa na kibenteni.


"Mimi siyo mwanamke wa kwanza kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye namzidi umri na siyo wa mwisho, dada zenu na mama zenu wanatoka na vibenteni, yani ikifikaga tu kwa Zari kila kitu kinakuwa ishu utazani mimi ndiyo mzee wa kwanza kuniona, kwani Tanzania hakuna wazee?"


"Yani miaka yangu 42 imekuwa gumzo Zari ni mzee ni mzee, kwani mimi ndiyo mzee wa kwanza? hamjawahi kuona wazee? wapo vibabu wanaotoka na watoto wa miaka chini ya 18 na hamsemi, dada zenu na mama zenu wanatoka na vitoto na hamsemi, midomo yenu imewakaa Zari Zarii, mnaboa sana Watanzania"- amelalamika Zari


"Siku nzima mnaniongelea Mimi, Mataifa mengine Huwa hawafatilii mambo kama hayo lakini nyie Sijuhi aliyewaroga," ameandika Zari.


Inafahamika kuwa, Zari na mwenzi wake Shakib wanapishana umri wa miaka 14.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad