Afande Rama Akutwa Hana Hatia, Aachiwa Huru




Mahakama ya Mkoa wa Vuga mjini Unguja Zanzibar imemuachia huru Mshtakiwa Ramadhan Ali ( Afande Rama) aliyekuwa akikaniliwa na kosa la kuruhusu kuingiliwa kuingiliwa kinyume na maumbile.

Mshtakiwa huyo mwenye kesi namba 59/ 2023 leo ameachiwa huru baada ya Hakimu Khamis Ali Simai wa Mahakama hiyo kudai Mshtakiwa hana hatia na amemuachia huru kwa kifungu cha 220 sheria namba 7 ya mwaka 2018.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Mwendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Mohamed Saleh ikiwa na jumla ya Mashahidi 9 wamewasilisha ushahidi ambao ushahidi wote haukuweza kumtia hatiani Mshtakiwa huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad