Ahmed Ally : Suala la Chama Lipo Kwa Viongozi


Kundi la pili la wachezaji wa klabu ya @simbasctanzania limeondoka alfajiri ya leo nchini kuelekea Uturuki kuungana na wachezaji wengine ambao tayari wapo huko wakiendelea na kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Katika wachezaji walioondoka hii leo, Clatous Chama amekosekana ambapo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, @ahmedally_ amesema "Chama hajaondoka na swala lake lipo kwa viongozi wa juu wakijaribu kulishughulikia lakini Chama hayupo kwenye safari hii ya kundi la pili la wachezaji wanaoelekea Uturuki".

Ahmed amesisitiza kuwa Mwamba wa Lusaka hana anachoidai klabu na bado ana mkataba na klabu hiyo wa mwaka mmoja hivyo amewatoa hofu wanachama na wapenzi wa @simbasctanzania kuwa bado ataendelea kuitumikia timu yake msimu ujao.

Kundi hilo la pili limejumuisha wachezaji kama Willy Essomba Onan, Che Fondoh Malone Jr, Jean Baleke na kocha wa viungo huku mchezaji Aubin Kramo Kouamé wataungana nae Ankara Esenboğa Airport

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad