Aliyekuwa Mtangazaji wa BBC Afariki Dunia


Mtangazaji Mkongwe wa Shirika la habari BBC George Alagiah (67), amefariki dunia.

Alagiah alifanya kazi katika televisheni kwa zaidi ya miaka 30, vilevile alitangaza taarifa ya habari ya BBC ya saa kumi na mbili kwa miaka 20 na kuwa mmoja wa waandishi walioheshimika sana.

Aliwahi kuripoti kutokea nchi mbalimbali ikiwemo Iraq na Rwanda.

Mtangazaji huyo mwenye asili ya Srilanka aligundulika na saratani ya utumbo mwaka 2014, kufikia mwaka jana alitangaza kuwa saratani yake imesambaa.

Taarifa kutoka kwa wakala wake imesema, Alagiah amefariki leo kwa utulivu akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake.

Mkurugenzi mkuu wa BBC, Tim Davies ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha mtangazaji huyo na ametuma salamu za rambirambi kwa familia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad