Aliyemuua Mwanafunzi UDOM naye Kunyongwa Hadi kufa




Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu Idris Mwangobola kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Happiness Mbonde.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Jaji Kisanya wa mahakama hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili ambapo amejiridhisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la mauaji kwa kukusudia.

Ilielezwa kuwa Idrisa alimuua Happiness kwa alichodai wivu wa mapenzi baada ya kubaini amepigiwa simu na mpenzi wake wa zamani na wakiwa chumbani kwake alifanya mapenzi na Happiness, kisha akampa juisi aliyoweka dawa za usingizi na baada ya binti huyo kuonesha kuchoka ndipo alimnyonga.

“Maelezo yanaonesha kuwa Idrisa alimuua Happines baada ya kupata hasira; hapo kifungu cha 201 cha kanuni ya adhabu hutumika. Maelezo lazima yathibitishe kuwa mauaji yalifanyika wakati mshtakiwa alipokuwa na hasira, lakini hiyo lazima mshtakiwa ahojiwe wakati ule ule baada tu ya tukio.


"Lakini kwa shauri hili, Happiness hakuuawa palepale baada ya mshtakiwa kuona amepigiwa simu na mpenzi wake wa zamani, hakuna kinachoshawishi kwamba aliuawa kwa hasira, bali inaonesha Idrisa alidhamiria,” alisema Jaji Kisanya.

Aliongeza kuwa “kwanza baada ya kunyonga, Idrisa alimwambia mama huyu anaumwa. Mshtakiwa alidhamiria na Jamhuri iliweza kuthibitisha hilo kwa mujibu wa kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya kanuni za adhabu.”

Kwa mujibu wa Jaji Kisanya, uchunguzi wa daktari pia unaonesha kuwa kifo cha Happiness kilitokana na kukosa hewa kwa kunyongwa.


Jaji Kisanya alisema awali mshtakiwa alikana kosa hilo ndipo akaamua kuisikiliza na Jamhuri ilileta mashahidi tisa na vielelezo kadhaa akiwemo baba wa marehemu (Fred Mbonde) aliyeweka muunganiko wa maelezo yake na tiketi ya kusafiria ya basi la Kimbinyiko aliyokata marehemu ambayo ilikutwa chumbani kwa mtuhumiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad