Aliyeongoza Majadiliano Kati ya Serikali na DP World Afunguka




Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, juu ya uwekezaji bandarini, Hamza Johar

MWENYEKITI wa Kamati ya Majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, juu ya uwekezaji bandarini, Hamza Johar amesema mvutano mkali uliibuka baina ya pande mbili kabla mkataba wa ushirikiano kuhusu suala hilo haujaingiwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza jijni Dar es Salaam, Leo tarehe 14 Julai 2023, Hamza amesema mvutano huo uliibuka katika baadhi ya vipengele, ikiwemo kinachohusu namna wazawa watashiriki kwenye uwekezaji.

Pamoja na namna DP World itakayosaidia nchi katika kupata utaalamu kuhusu uendeshaji bandari kisasa.

“Ibara ya 13 ya mkataba kuhusu ushirikishaji wafanyakazi, hii ilikuwa kidogo tushindwane nae. Tulisema awajali wafanyakazi atakaowakuta. Pia, tulimtaka atoe kipaumbele kwa kampuni za ndani na kusaidia kujenga vyuo vya mafunzo kama DMW na NIT,”


“Hapa alikataa tukasema kama hawataki basi, tulifanya hivi ilikuwa lazima tumtishe lakini baadae alikubali,” amesema Hamza.

Hamza amedai ” mkataba hauna tobo wala dosari yoyote na niko tayari kukaa popote kutoa ufafanuzi.”


Amesema katika mkataba wa makubaliano, kuna vipengele vinavyoelekeza DP World kusitishiwa mkataba endapo shughuli zake hazitaendeshwa kwa ufanisi au kukiuka mkataba huo.


“Ibara ya 22 imeweka vizuri kuwa mkataba utasitishika. Mkataba utasitishwa sababu Ibara ya 23 (1), inasema mkataba utasita pale miradi ya biashara na shughuli zitaisha. Na kule kwenye mikataba ya biashara kuna kipengele kinasema ukisitisha kule umesitisha na huku. Pia, pande zote mbili ziliozoingia mikataba lazima zitasitishwa,”amesema Hamza.

Hamza amedai DP World hajauziwa bandari, bali atakodishiwa kwa muda ambao utawekwa katika mikataba ya utekelezaji itakayoingiwa hivi karibuni.

Pia, amesema DP World atapewa asilimia nane ya sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam, na si Bandari nzima kama inavyodaiwa.


Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa
Amesema DP World kabla hajaanza kazi, atasajili Kampuni ya kitanzania na asilimia 35 za hisa atatoa kwa wazawa.


Kuhusu ibara ya 30 inayosisitiza mazingira ya sheria za nchi kutobadilika endapo mkataba huo utaanza kutekelezwa, Hamza amefafanua alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuweka Mazingira ya utulivu na kutoanzisha Kodi au tozo zitakazoathiri miradi kwa ajili ya kuvutia muwekezaji.

Amesema makubaliano hayo hayakungiwa ghafla, bali mchakato wake ulianza 2018.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad