Amuua Mkewe Baada ya Kumpima Mtoto DNA na Kubaini si Mwanaye

Amuua Mkewe Baada ya Kumpima Mtoto DNA na Kubaini si Mwanaye


Polisi katika Wilaya ya Mpigi nchini Uganda wanamshikilia Waeed Taheed (raia wa Israel) ambaye inasemekana alimuua mkewe na kuficha mabaki yake kwenye 'Tank' la maji taka.


Kwa mujibu wa polisi, Waeed Taheed, mkazi wa Kijiji cha Kalagala wilayani Mpigi na meneja wa karakana ya Reynolds Construction Company Ltd (RCC) iliyopo Kayabwe, wilayani humo, aliripoti kesi ya kupotea kwa mke wake Monica Nabukenya (25) Tarehe 16 Julai 2023.


Wakati wa Upelelezi, askari wa upelelezi wa Kituo cha Kayabwe walimuamuru Taheed awaongoze hadi nyumbani kwake, na baada ya kufika huko, harufu ya mwili uliokuwa ukioza ilisikika, baadaye alikiri kumuua mke kwa sababu aligundua Mtoto wa Miezi Sita sio Wake.


Hapo awali Inasemekana kwamba Taheed alimshuku Nabukenya kwa kutokuwa mwaminifu katika Ndoa, jambo ambalo lilimfanya amchukue mtoto wao wa miezi 6 kisha akampeleka kwenye kipimo cha (DNA) na matokeo yakawa hasi.


Baada ya hapo kulitokea sintofahamu Kwenye Familia hiyo, Kisha Bw. Taheed aliamua kumuua mkewe na kuutupa mwili wake kwenye 'Tank' la maji taka ndani ya Nyumba yao na kufunika maiti hiyo kwa udongo.


Jeshi la Polisi nchini Uganda bado linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hili la kikatiri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad