Anayetuhumiwa Kumchoma kwa Magunia ya Mkaa Mkewe Adai Haogopi Kunyongwa

 

Anayetuhumiwa Kumchoma kwa Magunia ya Mkaa Mkewe Adai Haogopi Kunyongwa

Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, amedai haogopi kunyongwa hadi kufa wala adhabu nyingine yoyote.


Hata hivyo, mshtakiwa huyo amedai kuwa anataka "anyongwe kwa haki" kwamba aliua bila kukusudia.


Katika kesi hiyo ya mauaji Na. 4 ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam, anadaiwa kuwa Mei 15, 2019, akiwa Gezaulole, Kigamboni, alimuua Naomi Marijani.


Luwonga alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhani Rugemalira wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dares Salaam baada ya kusomewa maelezo ya mashihidi 28 na vielelezo 14 na upande wa mashitaka.


"Kitu ambacho ninakikataa mheshimiwa hakimu, ni kuwa niliua kwa makusudi. Mimi sikuua kwa makusudi. Hata ninyongwe leo hadi kufa kwa kile cha kweli, nitaangamia kimwili lakini siyo kiroho.


"Siogopi kunyongwa wala siogopi adhabu yoyote ile, lakini ninataka kama nikinyongwa, basi ninyongwe kwa haki kwamba niliua bila kukusudia, kwa sababu ni ajali tu ilitokea," alidai Luwonga.


Hapo Hakim Rugemalira akaingilia akisema: "Unaanza kuhubiri sasa, wewe zungumza unachotaka kuzungumza ili nikiandike kwenye rekodi za mahakama."


Luwonga aliendelea kudai kuwa msingi wa kesi hiyo ni maelezo yake, baada ya kuwaambia polisi kwamba yeye ndiye aliyeua na ndiye aliyekuwa anajitumia ujumbe mfupi kutoka simu ya mkewe kwenda katika simu yake.


"Kama shetani angeendelea kunishikilia hadi leo hi, hakuna mtu angejua kitu nimefanya, lakini roho mtakatifu alinishukia na nilikuwa na sukumwa kusema ukweli. Kwa sababu nilikaa miezi miwili na siku moja bila ukweli kujulikana, hadi sasa Naomi asingejulikana yuko wapi.


"Kutokana na hofu ya Mungu, niliamua kusema ukwell sio kwa sababu nilipata mateso kutoka kwa askari polisi, hapana! Ni mimi mwenyewe niliamua," alidai Luwonga.


Mshtakiwa huyo pia aliiomba mahakama kuwa pindi kesi itakapoanza kusikilizwa, Mahakama Kuu ihamie sehemu ya tukio nyumbani kwake, ili wane mashimo sita aliyoyachimba katika nyumba zake sita na nyumba ya kulala wageni kwa ajili ya maji taka. Alidai kuwa lengo la mahakama kwenda eneo hilo ni ili ione mashimo yaliyochimbwa yalikuwa ni ya maji taka na sio kwa ajili ya kumzika mkewe, kwa sababu yeye ndiye alitaka kwa ajili ya maji machafu.


Ni madai yaliyomfanya hakimu aingilie, akisema: "Sasa mshitakiwa huko unapokwenda ni kwenye ushahidi. Hayo utayazungumza huko Mahakama Kuu katika ushahidi wako."


Mshitakiwa Luwonga alidai: "Mheshimiwa ninaomba ufahamu jambo moja; hawa mawakili wangu nimewaomba wanitetee kwa haki na siyo kupindishapindisha mambo kwa sababu mimi ndiye niliamua mwenyewe kuzungumza ukweli," alidai Luwonga.


Alidai hayo baada ya wakili wake, Mohamed Majaliwa kumtaka aache kuzungumza. Wakili huyo alimtaka wazungumze kwanza wao kabla ya yeye kuendelea kuzungumza mbele ya hakimu.


"Ninawaomba mawakili wa serikali, mnipelekee taarifa zangu kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwamba aharakishe kesi hi lishe haraka kwa sababu hata Rais na jamii kwa ujumla wanataka kujua mwisho wake kwa sababu kesi yangu hii ilitikisa chi.


"Ninataka kesi hii iwe fundisho kwa watu wengi, kwa sababu tulifanya uzembe mkubwa sana sisi wanandoa na jamii pia ilifanya uzembe hadi mauaji yakatokea, alidai Luwonga.


Baada ya mshitakiwa kudai hivyo, Hakimu Rugemalira alimweleza kwamba hakuna kesi kubwa. Zote zinalingana na hakuna kesi inayotikisa chi, hivyo hata kesi inayomkabili "sio konki" kama alivyodai. Mshitakiwa huyo alidai atakuwa na mashahidi 20 na atakuwa na vielelezo wakati shahidi unaendelea. Atavitoa mwenyewe au mashahidi wake watakuja navyo mahakamani.


"Una haki zako za msingi za kupewa wakili na kupewa orodha ya mashahidi, kama utahitaji na mawakili wako hawa wawapo, hilo ni jukumu lako wewe. Kwa hiyo, unahamishiwa kwenda Mahakama Kuu," alisema Hakimu Rugemalira.


Luwonga anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa na baadaye alichukua majivu ya mwili wa marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga mkoani Pwani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad