Auawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu shambani





MKAZI wa Kijiji Cha Merya Tarafa ya Ilongero wilayani Singida, Innocent Dube (49) ameuawa kwa kuchomwa kisu mgongoni baada ya kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu shambani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema, tukio hilo limetokea Julai 9, 2023.

Kufuatia Tukio hilo Jeshi la Polisi linamsaka Simon Mwangi (58) mkazi wa Ghata wilayani Singida anayedaiwa kuhusika na mauaji hayo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad