Baada ya Jonas MKUDE Kutua Kibabe Yanga, Huyu Ndie Anaefuata

 

Baada ya Jonas MKUDE Kutua Kibabe Yanga, Huyu Ndie Anaefuata

Nahodha wa AS Maniema Union ya DR Congo, Maxi Mpia amewasili nchini wa leo Julai 12, 2023 kukamilisha dili la kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Maxi kama mambo yataenda sawa msimu ujao atavaa uzi wa njano na kijani ambapo taarifa za kupenyezewa zinadai Yanga watalazimika kutumia zaidi ya Sh400 milioni kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia kwenye klabu yake ya AS Maniema.

Winga huyo anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Mkongomani mwenzake Twisila Kisinda aliyeimaliza mkataba wake wa mwaka wa mkopo akitokea RS Berkane ya Morocco.

HUKU KWA MKUDE KIMELEWEKA

Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kumsajili kiungo, Jonas Mkude kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.

Huu unakuwa ni usajili wa tatu wa Yanga msimu huu baada ya kumsajili Nickson Kibabage kutoka Singida FG na Gift Fred kutoka SC Villa ya Uganda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad