Baada ya Kusign Mwaka Mmoja Yanga, Jonas Mkude Apewa Tahadhari Gombania Namba na Sure Boy

 

Baada ya Kusign Mwaka Mmoja Yanga, Jonas Mkude Apewa Tahadhari Gombania Namba na Sure Boy
Jonas Mkude

Tetesi za Usajili Yanga

KITENDO cha kiungo mkabaji, Jonas Mkude kupewa mkataba wa mwaka mmoja Yanga ni kama mtego kwake na amepewa mtihani mzito wa kupambanishwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambaye msimu ulioisha alicheza kwa kiwango cha juu.

Miaka 11 aliyotumika Simba, Mkude alikuwa na vipindi vya mafanikio na changamoto mfano msimu ulioisha alikuwa na nafasi finyu ya kucheza, jambo lililowafanya watalamu wa soka wamwambie ni kitu gani akakifanye Yanga ili kurejesha thamani yake.

Staa wa zamani wa Simba, Mohamed Banka aliona changamoto atakayokabiliana nayo Mkude ni ushindani baina yake na Sure Boy, alimshauri mwaka mmoja aliopewa ukawe wa kujitoa zaidi ili wajenge imani naye ya kumuongezea muda zaidi.

“Nidhamu mbovu alizokuwa anatajwa nazo Simba akaachane nazo, umri wake unakwenda na ajue Yanga kila idala ina wachezaji wenye kiwango kikubwa, hivyo si rahisi kwake kuona anaweza akapata nafasi bila kujituma, labda ingekuwa kama Namungo ama Singida Big Stars huko ingetamba bila kikwazo.

“Ni mchezaji mzuri ni maamuzi yake mwenyewe kujifanyia tathimini ni vitu gani vilimfanya Simba asicheze msimu ulioisha akivifanyia kazi basi atarejea kwa kishindo na heshima yake itakaa kwenye mstari.”

Kwa upande wa beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah alisema Mkude ana kazi ya kuwaaminisha viongozi na mashabiki wa Yanga kuona hawajafanya makosa kumsajili ndani ya kikosi chao.

“Kilichomtokea kiliwahi kunitokea nilipotoka Yanga kwendan Simba nilipambana na kucheza kwa mafanikio hadi mashabiki wa Yanga wakaanza kuniona mimi ni Simba damudamu, hilo ndilo anapaswa kulionyesha Mkude akipambana atawashangaza wengi, hivyo si wakati wake kupumzika bali ajinoe kisawasawa ili awe fiti, atakapopewa nafasi akaonyeshe kinachostahili.

“Binafsi niliona bado huduma ya Mkude ilikuwa inahitajika Simba, sasa ajue msimu unaokuja utakuwa mgumu na wa presha kwake, kuna mashabiki wa kumzomea ila atapaswa kuwajibu kwa kiwango uwanjani maana ndio kazi yake, pia umri haurudi nyuma atulize akili kutimiza majukumu yake.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad