Basi Jingine la New Force Lapata Ajali Leo, Lapinduka Mlima Kitonga


Wiki moja tangu kutokea kwa ajali ya New Force iliyoua Watu saba na kujeruhi wengine 48 Mkoani Njombe wakati Dereva aki-overtake darajani, leo July 02,2023 Basi jingine la Newforce T448 DDT likitokea Iringa kwenda Dar es salaam limepata ajali eneo la Mlima kitonga wakati Dereva akilipita gari jingine.

@AyoTV_ imeongea na RPC wa Iringa Allan Bukumbi kwa njia ya simu na amethibitisha ajali ajali na kusema hakuna majeruhi wala kifo na kwamba basi hilo lilikuwa na abiria 57 na lilipinduka mara baada ya dereva kuyapita magari mengine na kushindwa kurudi katika mstari wake na ndipo alipogonga jiwe na gari hilo kupinduka.

“Kimsingi basi hilo lilikuwa linatokea Iringa kwenda Dar es salaam majira ya saa 3 na lilikuwa linashuka Mlima Kitomga na Dereva alikuwa anapita site ambayo siyo yake na alipoona mbele gari linakuja upande ambako yeye yuko alishindwa kulirudisha basi katika mstari wake ndipo alipogonga ngema ya mlima huo na basi hilo kupinduka ila abiria wote wameshuka salama”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad