Boti yazama Muleba, mmoja ahofiwa kufariki

Boti yazama Muleba, mmoja ahofiwa kufariki


Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amethibitisha Boti ya abiria kuzama katika Ziwa Victoria karibu na Kisiwa cha Kerebe kilichopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo amesema abiria walikuwa 26 na tayari Watu 25 wameokolewa wakiwa hai huku mtu mmoja akihofiwa kupoteza maisha.


DC huyo amesema; “Boti ilikuwa inatokea Kerebe kuelekea Bukoba ilipofika eneo moja maarufu linaitwa Mlango wanasema limekaa kama mlango wa kuingilia pale Kerebe na pana tatizo mara nyingi panakuwa na upepo mkubwa ambao huwa unavuma ndipo ilipozama"


"Abiria walikuwa 26 kati yao waliokolewa 25 wakiwa hai, wanne kati yao walipata hitilafu kidogo ya Afya wakapelekwa kwenye Zahanati na hivi ninavyozungumza wanaendelea vizuri, kwahiyo mmoja ndio huyo ambaye anahofiwa kupoteza maisha, nasema anahofiwa kupoteza maisha kwasababu mpaka dakika hii hatujapata udhibitisho kwamba mwili wake umepatikana ukiwa hai au laa!"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad