BREAKING: Yanga Wamtambulisha Mwenye Jezi Namba 6, Mwamba Huyu Hapa




Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo ya siku moja jijini Dar es Salaam, nyota wa Marumo Gallants, Mahlatse Makudubela amefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Yanga.

Winga huyo anayetumia hasa mguu wa kushoto alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu walioifikisha Marumo hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita ambayo walipoteza dhidi ya Yanga kwa kichjapo cha mabao 4-1 katika mechi mbili baina yao.

Yanga walianza kupiga hesabu za kumsajili mara baada ya kumuona katika mechi hizo mbili kabla ya leo kukamilisha usajili wake akitarajiwa kutambulishwa usiku majira ya 6:06.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Skudu alikuwa anatarajiwa kupewa jezi namba 6 ambayo iliachwa wazi na kiungo wa zamani wa Yanga Feisal Salum'Fei Toto' aliyeuzwa Azam FC.


Skudu alitua nchini jana usiku ambapo leo alikutana na viongozi wa Yanga kumalizia mazungumzo ya kuja kuitumikia timu hiyo.

Winga huyo anaweka rekodi ndani ya Yanga ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Afrika Kusini kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la Azam.

Usajili huo unaifanya Yanga hadi sasa kufikisha idadi ya wachezaji watano wapya iliowanasa katika dirisha hili kubwa la usajili.


Yanga tayari imeshawasainisha mabeki Nickson Kibabage, Gift Fred, kiungo Jonas Mkude, winga wa kulia Maxi Nzengeli na sasa Skudu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad