Cristiano Ronaldo 'Sina Mpango wa Kurudi Ligi ya Ulaya Wala ya Marekani, Ligi ya Saudi Arabia ni Bora zaidi"



Mshambuliaji wa klabu ya Al Nassr, Cristiano Ronaldo amesema kwamba Ligi kuu ya nchini Saudi Arabia ifahamikayo kama Saudia Pro League "ni bora" kuliko MLS ama "Major League Soccer" ya nchini Marekani, na kwamba mshambuliaji huyo wa Ureno hana mpango wa kucheza Marekani ama kurejea kwenye timu za barani Ulaya.

Ronaldo alizungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Celta Vigo ambapo klabu ya Al Nassr ilipoteza kwa bao 5-0 kwenye mechi ya maandalizi ya msimu mpya ikifanyika nchini Ureno.

Kwenye mazungumzo hayo Ronaldo alisema kuwa “Ligi ya Saudi Arabia ni bora kuliko ya Marekani” akijibu swali lililouliza kama angefikiria kuhamia Marekani kama mpinzani wake mkubwa Lionel Messi, ambaye alitambulishwa kama mchezaji wa Inter Miami siku ya Jumapili.

Ronaldo aliongeza kuwa “Hivi sasa wachezaji wote wanakuja Saudi Arabia, ndani ya mwaka mmoja, wachezaji wengi bora watakuja Saudi Arabia.”

Ronaldo alitolewa wakati wa mapumziko kipindi matokeo yakiwa 0-0, aliongeza kuwa "Nilifungua njia kuja ligi ya Saudia, na sasa wachezaji wengi wanakuja hapa.”

Ligi Kuu ya Saudi Arabia imeshuhudia mapokezi ya wachezaji wengi wakubwa kama mshindi wa Ballon d’Or Karim Benzema kutoka Real Madrid, N’Golo Kante kutoka Chelsea wote hawa wakijiunga na klabu ya Al-Ittihad. Kalidou Koulibary pamoja na Ruben Neves waliojiunga na klabu ya Al-Hilal, Roberto Firmino akijiunga na Al Ahli lakini pia kocha Steven Gerrard akichukua jukumu la kuinoa klabu ya Al-Ettifaq.

Ronaldo alihitimisha kwa kusema kuwa “Nina umri wa miaka 38 na nina uhakika 100% kwamba sitarejea katika klabu yoyote ya barani Ulaya.”

“Soka la Ulaya limepoteza ubora kwa kiasi kikubwa. Ligi pekee ambayo bado inafanya vizuri ni Ligi Kuu ya England, Wako mbele sana kuliko ligi zingine zote.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad