Daktari matatani kwa kutoa taarifa za mgonjwa aliyejikata uume




WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Mganga Mkuu wa Serikali kufanya uchunguzi na kubaini Daktari aliyetoa taarifa za Mgonjwa aliyejikata Uume za kuwa hatoweza tena kufanya tendo la ndoa, ili serikali imchukulie hatua stahiki na za kisheria daktari huyo.

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo mapema leo, Julai 13, 2023 wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utolewaji wa huduma za afya katika Mkoa wa Shinyanga na kuonesha kusikitishwa na mtu aliyetoa taarifa hiyo kwa ni kinyume na maadili katika Sekta ya Afya.

"Hapa naangalia kwenye Mitandao ya Kijamii naona kuna taarifa ya Mwanume kuwa amejikata uume na kwamba hataweza kufanya mapenzi tena, nimemuagiza Mganga Mkuu alifuatilie hilo nani katoa taarifa ya Mgonjwa," amesema Waziri Ummy.

Amesema si maadili utaoji wa taarifa za wagonjwa hayaruhusu kabisa kufanya hivyo na kuwasihi Madaktari na watoa huduma za Afya kuendelea kuzingatia Miiko ya taaluma zao,pamoja na kutumia lugha nzuri kuhudumia wagonjwa.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndugile, akisoma taarifa ya huduma za Afya mkoani humo, amesema upatikanaji wa huduma umeimarishwa pamoja na upatikaji wa dawa kwa zaidi ya asilimia 89.9.

Amesema licha ya huduma hizo kuboreshwa, lakini bado wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa watumishi na Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufani mkoani humo, pamoja na Magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance).

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, ameahidi kuendelea kutekeleza maelekezo ya serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa maadili kazini huku akimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kusimamia uboreshwaji wa huduma za afya mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad