Diamond Platnumz Afunika Maokoto Mirahaba Cosota


Usiku wa kuamkia leo Serikali kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) wamegawa Mirabaha kwa wasanii wa muziki hapa nchini.

Msanii @diamondplatnumz ameshika nafasi ya kwanza kwa kupata mgao wa Mirabaha wa TZS Milioni 7.7 akifuatiwa na @officialalikiba aliyevuna TZS Milioni 5 huku @rayvanny naye akikunja kitita cha TZS Milioni 4.9.

Mirabaha hiyo inatokana na makusanyo kutoka sehemu mbalimbali ambako kazi za wasanii nchini zimetumika kibiashara.

Wanufaika wengine katika Keki hiyo ni pamoja na Zuchu Milioni 4.7, Mbosso Milioni 4.3, Nandy Milioni 3.5, Harmonize Milioni 3.4, Maua Sama Milioni 2.3, Young Lunya Milioni 1.6.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad